Job 29:12-17

12 akwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,
naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
13 bMtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,
nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
14 cNiliivaa haki kama vazi langu;
uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
15 dNilikuwa macho ya kipofu
na miguu kwa kiwete.
16 eNilikuwa baba kwa mhitaji;
nilimtetea mgeni.
17 fNiliyavunja meno makali ya waovu,
na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
Copyright information for SwhNEN